Tuesday, May 3, 2011

Mei mosi Waziri asherehekea kwa kunywa kikombe

Na Thompson Mpanji,Chunya

Katika kusherehekea siku kuu ya wafanyakazi  mei mosi ambayo kitaifa ilifanyika mjini Morogoro,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri  ya muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete,huko wilayani Chunya  kuna  taarifa ya Waziri mmoja kuhitimisha  shamra shamra za sherehe hizo kwa kupata kikombe kutoka kwa mlemavu wa macho.

Akiongea na mwanablog hii Mkazi wa Kijiji cha Mbuyuni,Bw.Nico Haule amesema Naibu Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi,Mh.Philipo Mulugo jana alikuwa miongoni mwa wananchi waliokwenda kupata tiba ya  kikombe kutoka kwa  mpiga kura wake Mlemavu wa macho,Bw.Simon Mahela aliyedai  kuoteshwa na babu yake marehemu kutibu magonjwa yote sugu ikiwemo na ukimwi kwa muda wa siku 43.

Bw.Haule ambaye pia ni mdau wa masuala ya habari,amesema Bw.Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Songwe alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za mei mosi ambazo zilifanyika Chang’ombe,Kata ya Mbuyuni,wilayani Chunya ambapo baada ya kuhitimisha sherehe hizo kwa kutoa msaada wa Sh.200,000  ili kusaidia shughuli za mei mosi ziweze kuendelea yeye na makatibu wake wa jimbo walikwenda kushuhudia  tiba hiyo na hatimaye kupata  kikombe cha tiba na hivyo kukonga nyoyo za wapiga wake  na kumuona ni mwenzao.

Mlemavu huyo wa macho anatoa tiba hiyo  kwa masharti ya matamio ya siku 43 bila kunywa pombe wala kufanya tendo lolote la ndoa amekuwa akitoa huduma kwa familia nzima kuchangia sh.500 ambapo siku ya Ijumaa watoto na wanafunzi wanakunywa kikombe bure.

Hata hivyo Bw.Haule amesema  viongozi kadhaa wa Wilaya ya Chunya akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw.Deodatus Kinawiro ameshafika kupata tiba ya mlemavu huyo wakati alipokuwa katika ziara za kikazi.

Mwisho.




1 comment:

  1. Na Thompson Mpanji,Mbeya

    SERIKALI mkoani Mbeya imetoa mwito kwa wadau mbalimbali wa masuala ya kijamii jinsia na watoto kuzisaidia Asasi zisizo za kiserikali zinazojitoa kuisaidia jamii katika mazingira magumu kama ilivyo kwa Chama cha vijana wanawake wa kikristo Tanzania (YWCA),Tawi la Mbeya.

    Mwito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya,Evans Balama kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya John Mwakipesile ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya chakula cha pamoja na watoto yatima iliyofanyika makao makuu ya kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi(KMT),Jakaranda,jijini hapa.

    Balama amesema kabla ya kufika katika hafla hiyo alikuwa ameandaa hotuba yake kwa niaba ya mkuu wa Mkoa lakini baada ya kujionea shughuli inayofanywa na YWCA Mbeya kwa kujitolea na kuchangishana fedha na kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ameamua kutoa hotuba kufuatana na hali aliyoikuta.

    Aidha ameviomba vyombo vya habari kutumia nafasi yao kama vyombo vya jamii kuitangazia umma kuhusu shughuli zinazofanywa na Mashirika kama ya YWCA ili watu wenye nafasi kifedha pamoja na wadau mbalimbali waweze kujitokeza kuyasaidia.

    Mkuu huyo amesema YWCA Mbeya imekuwa ya mfano wa kuigwa na Asasi nyingine kutokana na ushiriki wao wa dhati na kujitoa kwa hali na mali kuifanyakazi ya kujitolea kuikoa jamii yenye uhitaji mkubwa kwa niaba ya serikali pasipo kusubiri kupata misaada kutoka kwa wafadhiri.

    Amefafanua kuwa pamoja na kuwepo maneno ya hapa na pale kuwa serikali haijafanya kitu kwa yatima na wahitaji wengine,jamii iwapuuzie kwani hawajuwi watendalo wala wasemalo kwani serikali inawajibika na kutambua mchango wa Asasi ndiyo maana haziwezi kufanyakazi bila kusajiliwa rasmi na serikali.

    Aidha kuhusu ujenzi wa Kijiji cha watoto yatima na wenye mtindio wa ubongo cha kambarage kinachojengwa na YWCA Mbeya,kilichopo Ivumwe jijini hapa Mkuu huyo wa wilaya amesema anafanya jitihada ya kuwatafuta wawekezaji ili waweze kukiendeleza ili lengo lilikusudiwa liweze kufikiwa na tayari ameshafanya mazungumzo na wawekezaji wawili ambao wameonesha nia.

    Kwa upande wake Katibu Mkuu wa YWCA Mbeya,Tawi la Mbeya,Tabitha Bughali akisoma risala amesema ujenzi wa kituo hicho unahitaji zaidi ya Sh.Bil.2 hadi kukamilika na tayari hatua za awali za ramani,tofari na msingi zimeshakamlika.

    Hata hivyo Bughali ameiomba serikali,Wadau mbalimbali na watu wenye mapenzi mema kuisaidia Asasi hiyo kwani imebeba mzigo mzito wa kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 199 ambapo 47 wanasomeshwa Sekondari,73 shule ya msingi na 79 katika vyuo vya ufundi.

    Amesema pamoja na vyanzo vya mapato ni michango na kuomba misaada kwa wahisani mbalimbali wanawahudumia pia watu wanaoishi na maambukizi ya virusi 13,wajane na wazee 12.

    Mwisho.

    ReplyDelete